huyo alisisitiza kuwa hakuhojiwa bali alipewa karatasi tupu na kutakiwa kusaini bila kufahamu ni kitu gani UNK 
 akielezea siku ya tukio alisema alipigiwa simu na ssp salum kisai ambaye alimtaka kufika katika ofisi za tume hiyo na alifika hapo oktoba kumi mwaka jana kutekeleza agizo la mpelelezi huyo 
 alidai kuwa baada ya kufika hapo aliambiwa na bwana kisai kuwa anahitaji kufanya marekebisho machache kwenye maelezo ya tuhuma zake hivyo alimpa karatasi tupu UNK na baadaye mpelelezi huyo angeandika maelezo 
 alidai kuwa kabla ya kutia saini aliruhusiwa kwenda msikitini kuswali hivyo aliondoka kuelekea maeneo ya mikocheni dar es salaam 
 sitasahau katika maisha yangu ni tukio la ajabu ambalo nilifanyiwa nikiwa msikitini alikuja ofisa mmoja wa tume na kunitaka niende ofisi zao huku mtoa hotuba akiwa amepanda eneo la kutolea hotuba hiyo kwa waislam ndicho kitu muhimu sana alidai bwana farijala